Created by: [email protected]
Gospelpopedmbluesenergeticmale voice

Music Images

Lyrics / Prompt

Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu. 2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.
Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya Roho. Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani. Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa kweli hawawezi. Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza Mungu .

Comments